NAPE ATUPA KIJEMBE KWA WAPINZANI....NI KUHUSU UPINZANI KUIANGUSHA CCM - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 12, 2018

NAPE ATUPA KIJEMBE KWA WAPINZANI....NI KUHUSU UPINZANI KUIANGUSHA CCM


Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye amefunguka na kusema upinzani nchini Tanzania hautaweza hata siku moja kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika madaraka kwa kuwa inapofika wakati wa kutafuta dola hawana urafiki na mtu. 

Nape Nnauye amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Longido kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambao unatarajiwa kufanyika kesho Januari 13, 2018. 

"Ikifika wakati wa kutafuta dola CCM inakuwa kitu kingine kabisa, unaweza kuichezea wakati wa kawaida na tunaweza kupiga stori ila ikifika kwenye kutafuta dola hapo ni mambo mengine kabisa. Ndiyo maana nasema wenzetu watasubiri sana kwani haiwezekani kuiangusha CCM madarakani" alisisitiza Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages