PICHA: HUYU HAPA KIGOGO WA CHADEMA ALIYEHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) LEO - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 9, 2018

PICHA: HUYU HAPA KIGOGO WA CHADEMA ALIYEHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) LEO

Kiongozi mkubwa wa upinzani aliyejiunga na CCM leo ni Muslim Hassanali aliyekuwa mgombea ubunge Ilala kwa tiketi ya Chadema mwaka 2015 .

Pia alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini na mmoja kati ya watia saini wa ruzuku za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kujiunga CCM.

Tayari viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na madiwani wamejiunga na CCM wakitokea upinzani kwa sababu tofautitofauti ikiwemo ya kuunga mkono serikali ya Rais John Magufuli.

Kiongozi huyo amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula akiwa na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es Salaam. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages