Jumanne ya leo Januari 9 Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na waziri mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa ikulu jijini Dar es salaam. Kitendo hicho kimepokelewa vizuri na watanzania walio wengi huku wengine wakidai kwamba kwa mara ya kwanza Afrika mashariki imetokea Tanzania pekee.
Miongoni mwa watanzania waliosifia kukutana kwa Rais Magufuli na Lowassa ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo hakusita kuelezea furaha yake.
Ridhiwani ameandika kupitia ukurasa wake wa instagram akisema.."Siasa hii ni Tanzania tu.Kwengine huko wanasubiri kukutanishwa.Hongereni sana Viongozi wa Ummma. Hongera sana Mheshimiwa Raisi kwa Hekima ya kuangalia Maendeleo ya Pamoja".

No comments:
Post a Comment