Rais wa Marekani Donald Trump amefanyiwa uchunguzi wa kiafya kwa mara ya kwanza tangu aanze kuiongoza nchi hiyo Januari 20, 2017.
Kituo cha BBC kimeripoti leo mchana kwa kusema kuwa taarifa kuhusu uchunguzi huo zimetolewa na daktari Ronny Jackson ambaye ni daktari wa Rais huyo wa Marekani.
Trump mwenye umri wa miaka 71 amefanyiwa uchunguzi huo siku ya Ijumaa Januari 12, 2018 na madaktari wa kijeshi, na kubaini kuwa ana afya nzuri kabisa.
Katika hatua nyingine Ronny Jackson amesema hakuna uchunguzi wa kiakili uliofanyika au kupangwa kufanyika licha ya kitabu cha Fire and Fury: Inside the Trump White House kilichoandikwa na Michael Wolf kutilia shaka akili ya Trump.
Mwandishi wa kitabu hicho anasema wafanyakazi wote wa White House wanamuona Trump kama mtoto mdogo anayefanya mambo yake bila kutumia akili.
No comments:
Post a Comment