SERIKALI KUANZA KULIPA MADENI YA NDANI KUANZIA MWEZI UJAO - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 4, 2018

SERIKALI KUANZA KULIPA MADENI YA NDANI KUANZIA MWEZI UJAO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kuwa mwezi ujao serikali itaanza kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa.

Rais Magufuli ameyasema hayo Ikulu, jijini Dar es Salaam, jana baada ya kuagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake, Prof. Benno Ndulu na kueleza kuwa, mwezi ujao Serikali itatoa Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa, yakiwemo ya wazabuni mbalimbali waliotoa huduma katika taasisi za Serikali, madai ya walimu na madai ya wakandarasi.

“Nasisitiza madeni tutakayolipa ni ya ndani, na tutalipa madeni ambayo yamehakikiwa, kwa hiyo maandalizi ya kutoa fedha hizo yaanze mara moja na ni matarajio yangu fedha hizi zitasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages