Athumani alipata ajali hiyo Agosti 12, 2008 katika eneo hilo wakiwa na waandishi wenzake njiani kwenda Kilwa. Baada ya hapo alibaki kitandani kwa matibabu Muhimbili, baadaye nchini Afrika Kusini hadi aliporejea nyumbani akiwa na anatumia kiti kutembelea.
Taarifa kutoka kwa ndugu zake zinasema jana mchana alizidiwa ghafla, wakampeleka Muhimbili ambalo alipata matibabu hadi mauti yanamkuta.
Mmoja wa wadau waliokuwa karibu naye tokea akiwa mzima wa afya enzi za uhai wake, Asha Baraka amesema tayari wameanza kufanya taratibu za mazishi na baadaye taarifa zitatolewa.
No comments:
Post a Comment