Taarifa za kusikitisha zinaeleza kuwa gari la kusafirishia mafuta limepinduka na kuungua moto maeneo ya mlima Sekenke mkoani Singida. Gari hilo lenye namba za usajili T.167 BQT pamoja na tela lake lenye namba T.960 ALX lilikuwa katika barabara kuu ya Singida/Nzega ambapo liliacha njia na kupinduka na hatimaye kuungua moto.
Tukio hili la kusikitisha limetokea leo majira ya saa nne asubuhi ambapo dreva wa gari hilo pamoja na tingo wake wanadaiwa kupoteza maisha.
Mukamafunny Blog imepata habari hizi kwa ufupi na tunasubiri taarifa kamili kutoka Jeshi la polisi ambao watakuwa na maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment