SAKATA LA KUMROGA BEN POL...EBITOKE AFUNGUKA UKWELI WOTE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 23, 2018

SAKATA LA KUMROGA BEN POL...EBITOKE AFUNGUKA UKWELI WOTE



Msanii wa filamu na mchekeshaji hapa bongo Ebitoke, ameweka wazi juu ya kufufuka kwa penzi lake na Ben Pol ambaye hapo awali alidai hapokei hata simu zake, na hivi karibuni kuanza kuwa pamoja tena.

Ebitoke amesema kwamba kitendo cha yeye kuonekana na Ben Pol kwenye kazi zake za comedy ni kwamba alishamuahidi kuwa atamsaidia kwenye kazi zake, na si ndumba kama baadhi ya watu wanavyodai, kutokana na kwamba penzi lao lilishakufa.

“Sijamroga Ben Pol, hata hivyo kipindi cha katikati ambacho mahusiano yetu hayakuwa sawa, sio kwamba hayakuwa sawa ni kwamba alinituliza nisiongee sana kwenye mitandao baada ya ile kusema hapokei simu zangu na kuwa niweze ku-manage mahusiano, tulikaa kama mwezi mzima tulikuwa hatuongelei chochote, lakini aliniahidi kuwa atanisaidia kazi ndo hivyo tunasaidiana”, amesema Ebitoke.

Wawili hao bado kuna sintofahamu kama ni kweli wapenzi, kwani mara nyingi Ben Pol amekuwa sio mtu wa kufurahia suala la mahusiano yake na Ebitoke kuwa wazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages