VIDEO: SHABIKI WA SIMBA ALIVYONUSURIKA KUFA BAADA YA KUPORA TAULO LA GOLIKIPA WA NJOMBE MJI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 4, 2018

VIDEO: SHABIKI WA SIMBA ALIVYONUSURIKA KUFA BAADA YA KUPORA TAULO LA GOLIKIPA WA NJOMBE MJI


Shabiki ambaye hakujulikana mara moja ameingia uwanjani kisha kukimbilia golini mwa mlinda mlango wa timu ya Njombe Mji, David Kisu na kuchukua taulo lililokuwa golini hapo kisha kukimbia nalo wakati timu hiyo ikicheza na Simba uwanja wa Sabasaba Njombe hii leo

Shabiki huyo anayedhaniwa kuwa ni wa Simba, amelipora taulo hilo na kuruka uzio wa uwanja huo na kukimbia nalo hali iliyozua taharuki uwanjani hapo

Shabiki huyo amekamatwa nje ya uwanja na kuanza kupokea kipigo kidogo kabla ya kuokolewa na askari polisi waliokuwa uwanjani hapo, huku taulo hilo likichomwa moto jambo ambalo limefanyika haraka kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na polisi

Zaidi Tazama Video hii hapa chini:-

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages